2 Chronicles 24:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za Mwenyezi Mungu? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha Mwenyezi Mungu, naye amewaacha ninyi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Roho wa BWANA akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za BWANA? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Roho wa bwana akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za bwana? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha bwana, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama mbele ya watu palikuwa juu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwa nini ninyi mnazivunja amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, roho ya Mungu ilipomwingia Zakaria, mwana wa mtambikaji Yoyada, akaja kusimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia: Hivi ndivyo, Mungu anavyosema: Mbona mnayaacha maagizo ya Bwana, msiendelee kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, naye amewaacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Roho wa Mungu akamujaza Zakaria mwana wa kuhani Yoyada, naye akasimama mbele ya watu kwa pahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia: “Yawe anauliza: Kwa nini mumevunja sheria zake? Sasa hamuwezi kufanikiwa! Kwa vile mumemwacha, naye vilevile amewaacha!”