2 Chronicles 24:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Yoashi aliyasahau mema yote aliyotendewa na Yehoyada, baba yake Zekaria, akamuua mwanawe. Alipokuwa anakufa, alisema, “Mwenyezi-Mungu na ayaone matendo yenu, akalipize kisasi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria, ila alimuua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “Mwenyezi Mungu na alione hili na alipize kisasi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, Bwana na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Yoashi aliyasahau mema yote aliyotendewa na Yehoyada, baba yake Zekaria, akamuua mwanawe. Alipokuwa anakufa, alisema, “Mwenyezi-Mungu na ayaone matendo yenu, akalipize kisasi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimwua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “BWANA na alione hili na alipize kisasi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimuua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “ bwana na alione hili na alipize kisasi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Yoashi aliyasahau mema yote aliyotendewa na Yehoyada, baba yake Zekaria, akamuua mwanawe. Alipokuwa anakufa, alisema, “Mwenyezi-Mungu na ayaone matendo yenu, akalipize kisasi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme Yoasi alipoacha kuyakumbuka matendo yote ya upole, baba yake Yoyada aliyomfanyizia, naye akamwua mwanawe; huyu alipokufa akasema: Bwana na ayaone na kuyalipisha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Yoasi akasahau mema yote aliyotendewa na Yoyada, baba ya Zakaria, akamwua mwana wake. Alipokuwa karibu kufa, alisema: “Yawe uangalie mambo haya na kuyalipiza.”