2 Chronicles 24:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuua kitandani mwake. Hivyo akafa, wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemwua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamwulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwenda zao, wakamwacha mwenye magonjwa mengi; ndipo, watumishi wake walipomlia njama, kwa kuwa alizimwaga damu za wana wa mtambikaji Yoyada, wakamwua kitandani pake, akafa; kisha wakamzika mjini mwa Dawidi, lakini hawakumzika penye makaburi ya wafalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui walipoondoka, wakamwacha akiwa ameumizwa vibaya sana, wakubwa wake wakamufanyia shauri baya, wakamwua juu ya kitanda chake, kwa kulipiza kisasi cha mauaji ya mwana wa kuhani Yoyada. Alizikwa katika muji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme.