2 Chronicles 24:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akawaita makuhani na Walawi na kuwaamuru, “Nendeni katika miji ya Yuda, mkusanye fedha kutoka kwa Waisraeli wote ili kurekebisha nyumba ya Mungu wenu kila mwaka; harakisheni.” Lakini Walawi hawakuharakisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni mijini mwa Yuda, mkakusanye katika Israeli wote fedha, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Walakini Walawi hawakuliharakisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akawaita makuhani na Walawi na kuwaamuru, “Nendeni katika miji ya Yuda, mkusanye fedha kutoka kwa Waisraeli wote ili kurekebisha nyumba ya Mungu wenu kila mwaka; harakisheni.” Lakini Walawi hawakuharakisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni katika miji ya Yuda, mkakusanye fedha kutoka Israeli wote, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Lakini Walawi hawakuliharakisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akawaita makuhani na Walawi na kuwaamuru, “Nendeni katika miji ya Yuda, mkusanye fedha kutoka kwa Waisraeli wote ili kurekebisha nyumba ya Mungu wenu kila mwaka; harakisheni.” Lakini Walawi hawakuharakisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawakusanya watambikaji na Walawi, akawaambia: Tokeni, mwende katika miji yote ya Yuda, mkusanye kwa Waisiraeli wote fedha za kuitengeneza Nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka! Neno hili na mlifanye kwa upesi! Lakini Walawi hawakulifanya kwa upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni mijini mwa Yuda, mkakusanye katika Israeli wote fedha, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Walakini Walawi hawakuliharakisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akawaita makuhani na Walawi na kuwaamuru: “Mwende katika miji ya Yuda, mukusanye feza kutoka kwa Waisraeli wote kwa kujenga upya nyumba ya Mungu wenu kila mwaka. Mufanye haraka.” Lakini Walawi hawakufanya haraka.