2 Chronicles 24:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme akamwita kiongozi Yehoyada, akamwuliza, “Mbona hujaamrisha Walawi kukusanya kutoka kwa watu wa Yuda na Yerusalemu, kodi ambayo Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliagiza watu walipe kwa ajili ya Hema Takatifu la Mwenyezi-Mungu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada kuhani mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema la Ushuhuda?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa Bwana, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme akamwita kiongozi Yehoyada, akamwuliza, “Mbona hujaamrisha Walawi kukusanya kutoka kwa watu wa Yuda na Yerusalemu, kodi ambayo Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliagiza watu walipe kwa ajili ya Hema Takatifu la Mwenyezi-Mungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada Kuhani Mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Mose mtumishi wa BWANA pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada kuhani mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Musa mtumishi wa bwana pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme akamwita kiongozi Yehoyada, akamwuliza, “Mbona hujaamrisha Walawi kukusanya kutoka kwa watu wa Yuda na Yerusalemu, kodi ambayo Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliagiza watu walipe kwa ajili ya Hema Takatifu la Mwenyezi-Mungu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipomwita Yoyada aliyekuwa mkuu wao, akamwambia: Mbona hukuwafuatafuata Walawi, watoze Wayuda na Wayerusalemu machango, aliyoyaagiza Mose, mtumishi wa Bwana, mkutano wa Waisiraeli wayachangie Hema la Ushahidi, kisha wayalete huku?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mufalme akamwita kiongozi Yoyada, akamwuliza: “Mbona haujaamurisha Walawi kukusanya kutoka kwa watu wa Yuda na Yerusalema, kodi ambayo Musa mutumishi wa Yawe aliagiza watu walipe kwa ajili ya Hema Takatifu la Yawe?”