2 Chronicles 25:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huohuo, wale wanajeshi Waisraeli ambao Amazia aliwaachia warudi kwao akiwakataza wasiandamane naye vitani, walikwenda na kuishambulia miji ya Yuda, toka Samaria hadi Beth-horoni, wakaua watu 3,000 na kuteka nyara nyingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo, wanajeshi waliorudishwa na Amazia, ambao hakuwaruhusu kushiriki katika vita, walivamia miji ya Yuda kuanzia Samaria hata Beth-Horoni. Wakawaua watu elfu tatu na kuchukua nyara nyingi sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wale watu wa jeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huohuo, wale wanajeshi Waisraeli ambao Amazia aliwaachia warudi kwao akiwakataza wasiandamane naye vitani, walikwenda na kuishambulia miji ya Yuda, toka Samaria hadi Beth-horoni, wakaua watu 3,000 na kuteka nyara nyingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo yale majeshi Amazia aliyoyarudisha na ambayo hakuyaruhusu kushiriki katika vita, yalivamia miji ya Yuda kuanzia Samaria hata Beth-Horoni. Yakawaua watu 3,000 na kuchukua kiasi kikubwa sana cha mateka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo yale majeshi Amazia aliyoyarudisha na ambayo hakuyaruhusu kushiriki katika vita, yalivamia miji ya Yuda kuanzia Samaria hata Beth-Horoni. Yakawaua watu 3,000 na kuchukua kiasi kikubwa sana cha mateka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wanajeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huohuo, wale wanajeshi Waisraeli ambao Amazia aliwaachia warudi kwao akiwakataza wasiandamane naye vitani, walikwenda na kuishambulia miji ya Yuda, toka Samaria hadi Beth-horoni, wakaua watu 3,000 na kuteka nyara nyingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wa kile kikosi, Amasia alichokirudisha, wasiende naye kupigana, waliingia miji ya Yuda toka Samaria hata Beti-Horoni, na kunyang'anya mali, wakapiga humo watu 3000, wakachukua mali nyingi, walizozinyang'anya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wale watu wa jeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati uleule, wale waaskari Waisraeli ambao Amazia aliwaacha warudi kwao akiwakataza wasijiunge naye katika vita, wakakwenda na kuishambulia miji ya Yuda, toka Samaria mpaka Beti-Horoni, wakaua watu elfu tatu na kunyanganya vitu vingi.