2 Chronicles 25:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Amazia mfalme wa Yuda alifanya shauri, akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akamwambia, “Njoo tupambane.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Amazia mfalme wa Yuda kushauriana na washauri wake, akatuma ujumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, kusema: “Njoo tukabiliane uso kwa uso.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme Amazia akafanya shauri, akatuma wajumbe kwa Yehoashi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Amazia mfalme wa Yuda alifanya shauri, akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akamwambia, “Njoo tupambane.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Amazia mfalme wa Yuda kushauriana na washauri wake akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli kusema: “Njoo tukabiliane uso kwa uso.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Amazia mfalme wa Yuda kushauriana na washauri wake akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli kusema: “Njoo tukabiliane uso kwa uso.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme Amazia akafanya shauri, akatuma wajumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, kusema, Njoo, tutazamane uso kwa uso.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Amazia mfalme wa Yuda alifanya shauri, akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akamwambia, “Njoo tupambane.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Amasia, mfalme wa Yuda, akapiga shauri, akatuma kwa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Waisiraeli, kumwambia: Njoo, tuonane uso kwa uso!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme Amazia akafanya shauri, akatuma wajumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, kusema, Njoo, tutazamane uso kwa uso.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Amazia mufalme wa Yuda alifanya shauri, akatuma ujumbe kwa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mwana wa Yehu mufalme wa Israeli, akamwambia: “Kuja tuonane uso kwa uso.”