2 Chronicles 25:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yoashi mfalme wa Israeli alimpelekea ujumbe Amazia akisema, “Siku moja, mchongoma wa Lebanoni uliuambia mwerezi wa hukohuko Lebanoni, ‘Mwoze binti yako kwa mwanangu!’ Lakini mnyama mmoja wa mwituni akapita hapo na kuukanyagakanyaga mchongoma huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, kusema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ukatuma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yoashi mfalme wa Israeli alimpelekea ujumbe Amazia akisema, “Siku moja, mchongoma wa Lebanoni uliuambia mwerezi wa hukohuko Lebanoni, ‘Mwoze binti yako kwa mwanangu!’ Lakini mnyama mmoja wa mwituni akapita hapo na kuukanyagakanyaga mchongoma huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, “Mbaruti uliokuwa huko Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa huko Lebanoni kusema, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa huko Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, kusema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ukatuma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita mnyama wa mwituni aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yoashi mfalme wa Israeli alimpelekea ujumbe Amazia akisema, “Siku moja, mchongoma wa Lebanoni uliuambia mwerezi wa hukohuko Lebanoni, ‘Mwoze binti yako kwa mwanangu!’ Lakini mnyama mmoja wa mwituni akapita hapo na kuukanyagakanyaga mchongoma huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akatuma kwa Amasia, mfalme wa Wayuda, kumwambia: Kingugi kilichoko Libanoni kilituma kwa mwangati ulioko Libanoni kwamba: Mpe mwanangu mtoto wako wa kike, awe mkewe! Ndipo, nyama wa porini wa huko Libanoni alipopita, akakikanyaga kile kingugi na kukiponda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, kusema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ukatuma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yoasi mufalme wa Israeli akamupelekea Amazia ujumbe akisema: “Siku moja, muti wa mubaruti wa Lebanoni ukauambia mwerezi nao ni wa kule hivi: ‘Umwoeshe binti yako kwa mwana wangu!’ Lakini nyama mumoja wa pori akapita pale na kukanyagakanyaga mubaruti ule.