2 Chronicles 25:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya matukio mengine katika utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya matukio mengine katika utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo mengine ya Amasia, ya mwanzo na ya mwisho, hatuyaoni, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo mpaka mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli.