2 Chronicles 25:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuanzia wakati Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata Mwenyezi Mungu, walipanga njama dhidi yake huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi. Lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi, nao wakamuua huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata Bwana, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuanzia wakati ule Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata BWANA walifanya shauri baya dhidi yake huko Yerusalemu naye akakimbilia Lakishi, lakini wakatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamwulia huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuanzia wakati ule Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata bwana walifanya shauri baya dhidi yake huko Yerusalemu naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamuulia huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu hapo, Amasia alipoacha kumfuata Bwana, walikuwako watu huko Yerusalemu waliomlia njama ya kumwua; kwa hiyo akakimbilia Lakisi, lakini wale wakatuma watu kumfuata lakisi, nao wakamwua huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mashauri mabaya ya kumwua Amazia yalifanywa Yerusalema tangu alipomwacha Yawe, kwa hiyo akakimbilia Lakisi. Lakini waadui wakatuma watu Lakisi wakamwua kule.