2 Chronicles 25:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hakuwaua watoto wao, kama ilivyoandikwa katika sheria zilizomo katika kitabu cha Mose, ambapo Mwenyezi-Mungu anasema: “Wazazi hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya wazazi wao; bali kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati, katika Kitabu cha Musa, ambako Mwenyezi Mungu aliamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya sawasawa na hayo yaliyoandikwa katika torati, katika kitabu cha Musa, kama Bwana alivyoamuru, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hakuwaua watoto wao, kama ilivyoandikwa katika sheria zilizomo katika kitabu cha Mose, ambapo Mwenyezi-Mungu anasema: “Wazazi hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya wazazi wao; bali kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na yaliyoandikwa kwenye Sheria, katika kitabu cha Mose, mahali BWANA alipoamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati, katika Kitabu cha Musa, ambako bwana aliamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya kulingana na hayo yaliyoandikwa katika Torati, katika kitabu cha Musa, kama BWANA alivyoamuru, akisema, Wazazi wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya watoto wao wala watoto wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya wazazi; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hakuwaua watoto wao, kama ilivyoandikwa katika sheria zilizomo katika kitabu cha Mose, ambapo Mwenyezi-Mungu anasema: “Wazazi hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya wazazi wao; bali kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wana wao hakuwaua, kwa kuwa katika Maonyo katika kitabu cha Mose imeandikwa, ya kuwa Bwana ameagiza kwamba: Baba wasife kwa ajili ya wana, wala wana wasife kwa ajili ya baba, ila kila mtu sharti afe kwa kosa lake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya sawasawa na hayo yaliyoandikwa katika torati, katika kitabu cha Musa, kama BWANA alivyoamuru, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hakuwaua watoto wao, kama vile ilivyoandikwa katika sheria zinazokuwa katika kitabu cha Musa, ambamo Yawe anatoa amri akisema: “Wazazi hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya wazazi wao; lakini kila mutu atauawa kwa ajili ya zambi zake mwenyewe.”