2 Chronicles 25:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Amazia aliwakusanya wanaume wa makabila ya Yuda na Benyamini, akawapanga katika vikosi mbalimbali kulingana na koo zao, akawaweka chini ya makamanda wa maelfu na wa mamia. Alipowakagua wale wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, alipata jumla ya watu 300,000. Wote walikuwa watu wateule, tayari kwa vita, hodari wa kutumia mikuki na ngao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume elfu mia tatu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, wenye uwezo wa kutumia mkuki na ngao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka sawasawa na nyumba za baba zao chini ya maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule mia tatu elfu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Amazia aliwakusanya wanaume wa makabila ya Yuda na Benyamini, akawapanga katika vikosi mbalimbali kulingana na koo zao, akawaweka chini ya makamanda wa maelfu na wa mamia. Alipowakagua wale wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, alipata jumla ya watu 300,000. Wote walikuwa watu wateule, tayari kwa vita, hodari wa kutumia mikuki na ngao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume 300,000 watu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, walio na uwezo wa kutumia mkuki na ngao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume 300,000 watu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, walio na uwezo wa kutumia mkuki na ngao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Amazia aliwakusanya wanaume wa makabila ya Yuda na Benyamini, akawapanga katika vikosi mbalimbali kulingana na koo zao, akawaweka chini ya makamanda wa maelfu na wa mamia. Alipowakagua wale wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, alipata jumla ya watu 300,000. Wote walikuwa watu wateule, tayari kwa vita, hodari wa kutumia mikuki na ngao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Amasia akawakusanya Wayuda, akawapanga kwa milango na kwa wakuu wa maelfu na kwa wakuu wa mamia wote pia waliokuwa Wayuda na Wabenyamini. Alipowakagua walio wenye miaka ishirini na zaidi akapata watu 300000 waliochaguliwa kwenda vitani waliojua kushika mikuki na ngao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka sawasawa na nyumba za baba zao chini ya maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule mia tatu elfu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Amazia akawakusanya wanaume wa Yuda, akawapanga katika vikundi mbalimbali kulingana na ukoo zao, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na wa mamia kwa ajili ya Yuda na Benjamina. Alipowakagua wale wenye miaka makumi mbili na zaidi, akapata watu elfu mia tatu kwa jumla. Wote walikuwa watu waliochaguliwa wanaofaa kwa vita, wanaoweza kutumia mikuki na ngao.