2 Chronicles 25:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaajiri pia wapiganaji elfu mia moja kutoka Israeli kwa talanta mia moja za fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaajiri pia watu mashujaa mia elfu wa Israeli kwa talanta mia za fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaajiri pia watu 100,000 wapiganaji kutoka Israeli kwa talanta 100 za fedha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaajiri pia watu 100,000 wapiganaji kutoka Israeli kwa talanta 100 za fedha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaajiri pia watu mashujaa elfu mia moja wa Israeli kwa talanta mia moja za fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajipatia nako kwa Waisiraeli watu wa mshahara 100000 waliokuwa mafundi wa vita wenye nguvu, akawalipa vipande mia vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaajiri pia watu mashujaa mia elfu wa Israeli kwa talanta mia za fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, alilipa waaskari wengine mashujaa elfu moja kutoka Israeli, kwa bei ya kilo elfu tatu za feza.