2 Chronicles 25:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amazia akamwuliza huyo mtu wa Mungu, “Tutafanyaje na fedha yote ambayo nimekwisha wapa wanajeshi wa Israeli?” Naye akamjibu, “Mwenyezi-Mungu anaweza kukupa zaidi ya hiyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amazia akamuuliza yule mtu wa Mungu, “Lakini itakuwaje kwa zile talanta mia moja za fedha nilizolipa kwa ajili ya haya majeshi ya Israeli?” Yule mtu wa Mungu akajibu, “Mwenyezi Mungu aweza kukupa zaidi ya hizo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Bwana aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amazia akamwuliza huyo mtu wa Mungu, “Tutafanyaje na fedha yote ambayo nimekwisha wapa wanajeshi wa Israeli?” Naye akamjibu, “Mwenyezi-Mungu anaweza kukupa zaidi ya hiyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amazia akamwuliza yule mtu wa Mungu, “Lakini itakuwaje kwa zile talanta 100 za fedha nilizolipa kwa ajili ya haya majeshi ya Israeli?” Yule mtu wa Mungu akajibu, “BWANA aweza kukupa zaidi sana ya hizo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amazia akamuuliza yule mtu wa Mungu, “Lakini itakuwaje kwa zile talanta 100 za fedha nilizolipa kwa ajili ya haya majeshi ya Israeli?” Yule mtu wa Mungu akajibu, “ bwana aweza kukupa zaidi sana ya hizo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amazia akamwuliza huyo mtu wa Mungu, “Tutafanyaje na fedha yote ambayo nimekwisha wapa wanajeshi wa Israeli?” Naye akamjibu, “Mwenyezi-Mungu anaweza kukupa zaidi ya hiyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amasia akamwuliza huyu mtu wa Mungu: Tena nivifanyeje vile vipande mia vya fedha, nilivyowapa wao wa kikosi cha Waisiraeli? Ndipo, huyu mtu wa Mungu alipomwambia: Bwana anaweza kukupa zaidi ya hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amazia akamwuliza yule mutu wa Mungu: “Tutafanya nini na feza yote ambayo nimekwisha wapa waaskari wa Israeli?” Naye akamujibu: “Yawe anaweza kukupa zaidi ya hiyo.”