2 Chronicles 26:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata nyikani pia alijenga minara, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na mifugo mingi kwenye sehemu za miinuko na tambarare. Alikuwa na wakulima wa watunza mizabibu milimani, na katika ardhi yenye rutuba kwani alipenda kilimo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilima na katika nchi tambarare. Alikuwa na watu waliofanya kazi katika mashamba yake, na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabirika mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata nyikani pia alijenga minara, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na mifugo mingi kwenye sehemu za miinuko na tambarare. Alikuwa na wakulima wa watunza mizabibu milimani, na katika ardhi yenye rutuba kwani alipenda kilimo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilimani na kwenye nchi tambarare. Alikuwa na watu wanaofanya kazi katika mashamba yake na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilimani na kwenye nchi tambarare. Alikuwa na watu wanaofanya kazi katika mashamba yake na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata nyikani pia alijenga minara, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na mifugo mingi kwenye sehemu za miinuko na tambarare. Alikuwa na wakulima wa watunza mizabibu milimani, na katika ardhi yenye rutuba kwani alipenda kilimo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata nyikani akajenga minara, akachimba visima vingi, kwani alikuwa na makundi mengi katika nchi ya tambarare, nako kwenye mbuga; akawa na wakulima na watunza mizabibu milimani na mashambani kwenye wiva, kwani alipenda kazi za ulimaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabirika mengi, maana alikuwa na ng’ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata katika jangwa vilevile alijenga minara, akachimba visima vingi, maana alikuwa na makundi mengi ya nyama kwenye sehemu za miinuko na mabonde. Alikuwa na walimaji na watunza mizabibu kwenye milima, na katika inchi yenye mboleo maana alipenda mulimo.