2 Chronicles 26:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mfalme Uzia alipokuwa na nguvu, alijaa kiburi ambacho kilisababisha maangamizi yake. Alimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake kwa kuingia hekaluni akikusudia kufukiza ubani madhabahuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa Mwenyezi Mungu ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi Bwana, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa Bwana, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mfalme Uzia alipokuwa na nguvu, alijaa kiburi ambacho kilisababisha maangamizi yake. Alimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake kwa kuingia hekaluni akikusudia kufukiza ubani madhabahuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa BWANA Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa BWANA ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa bwana Mwenyezi Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa bwana ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mfalme Uzia alipokuwa na nguvu, alijaa kiburi ambacho kilisababisha maangamizi yake. Alimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake kwa kuingia hekaluni akikusudia kufukiza ubani madhabahuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipopata nguvu, moyo wake ukajikuza, afanye yasiyofanywa, akamvunjia Bwana Mungu wake maagano akiingia Jumbani mwa Bwana kumvukizia mezani pa kuvukizia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakati mufalme Uzia alipokuwa na nguvu, moyo wake akajaa kiburi ambacho kilisababisha maangamizi yake. Akamwasi Yawe wake kwa kuingia ndani ya hekalu akikusudia kufukiza ubani juu ya mazabahu.