2 Chronicles 26:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uzia, aliyekuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ukoma ukamtokea kwenye paji la uso wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaghadhibika Uzia; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowaghadhibikia makuhani, ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana karibu na madhabahu ya kufukizia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la BWANA, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la bwana, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uzia akakasirika; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowakasirikia makuhani, ukoma ukamtokea katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa BWANA karibu na madhabahu ya kufukizia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Uzia alipochafuka, nacho kivukizio cha kuvukizia kilikuwa mkononi mwake; alipowatolea watambikaji machafuko yake, ukoma ukamtoka pajini pake usoni pa watambikaji mle Nyumbani mwa Bwana kando ya meza ya kuvukizia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaghadhibika Uzia; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowaghadhibikia makuhani, ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa BWANA karibu na madhabahu ya kufukizia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Uzia alikuwa amesimama ndani ya hekalu karibu na mazabahu, akishika chetezo cha kufukizia ubani katika mukono. Akawakasirikia makuhani; na mara tu alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.