2 Chronicles 26:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Uzia akawa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee kwani hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Naye Yothamu mtoto wake, akatunza jamaa yake huku akitawala wakazi wa nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Uzia alikuwa na ukoma hadi siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la mfalme, pia akawaongoza watu wa nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uzia mfalme akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya Bwana; na Yothamu mwanawe alikuwa juu ya nyumba ya mfalme, akiwahukumu watu wa nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Uzia akawa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee kwani hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Naye Yothamu mtoto wake, akatunza jamaa yake huku akitawala wakazi wa nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Uzia alikuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la BWANA. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la kifalme, pia akawaongoza watu wa nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Uzia alikuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la bwana. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la mfalme, pia akawaongoza watu wa nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme Uzia akawa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee kwani hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Naye Yothamu mtoto wake, akatunza jamaa yake huku akitawala wakazi wa nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme Uzia akawa mwenye ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa akiwa mwenye ukoma katika nyumba ya wagonjwa waliotengwa, kwani alikatazwa kuiingia Nyumba ya Bwana, mwanawe Yotamu akawa mkuu nyumbani mwa mfalme, akawaamua watu wa nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uzia mfalme akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa juu ya nyumba ya mfalme, akiwahukumu watu wa nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mufalme Uzia akakuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee maana hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Yawe. Na Yotamu mutoto wake, akatunza jamaa yake akitawala wakaaji wa inchi.