2 Chronicles 27:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Uzia baba yake; isipokuwa yeye hakuingia katika hekalu la Mwenyezi-Mungu nao watu waliendelea kufanya maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa Bwana. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Uzia baba yake; isipokuwa yeye hakuingia katika hekalu la Mwenyezi-Mungu nao watu waliendelea kufanya maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA kama vile Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa BWANA. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafanya yaliyo mema machoni pa bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama alivyofanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu waliendelea kufanya maovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Uzia baba yake; isipokuwa yeye hakuingia katika hekalu la Mwenyezi-Mungu nao watu waliendelea kufanya maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama yote, aliyoyafanya baba yake Uzia, namo Jumbani mwa Bwana hakuingia; lakini watu wakaendelea kuyafanya yasiyofanywa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitenda kwa usawa mbele ya Yawe kama vile Uzia baba yake alivyotenda. Hakuingia katika hekalu la Yawe. Watu waliendelea kufanya maovu.