2 Chronicles 27:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipigana vita dhidi ya mfalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka huo Waamoni walimtolea ushuru wa kilo 3,400, tani 1,000 za ngano na kilo 1,000 za shayiri; waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, na kori elfu kumi za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akapigana na mfalme wa wana wa Amoni, akawashinda. Na wana wa Amoni wakampa mwaka ule ule talanta mia za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea wana wa Amoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipigana vita dhidi ya mfalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka huo Waamoni walimtolea ushuru wa kilo 3,400, tani 1,000 za ngano na kilo 1,000 za shayiri; waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 100 za fedha, kori 10,000 za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 100 za fedha, kori 10,000 za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akapigana na mfalme wa Waamoni, akawashinda. Na Waamoni wakampa mwaka ule ule talanta mia moja za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea Waamoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipigana vita dhidi ya mfalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka huo Waamoni walimtolea ushuru wa kilo 3,400, tani 1,000 za ngano na kilo 1,000 za shayiri; waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena akapiga vita na mfalme wa wana wa Amoni akawashinda. Kwa hiyo wana wa Amoni hawakuwa na budi kumpa katika mwaka huo vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000 na ngano frasila 100000 na mawele vilevile frasila 100000. Hata mwaka wa pili na wa tatu wana wa Amoni wakamtolea yayo hayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akapigana na mfalme wa wana wa Amoni, akawashinda. Na wana wa Amoni wakampa mwaka ule ule talanta mia za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea wana wa Amoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipigana vita na mufalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka ule Waamoni wakamutolea kodi ya kilo elfu tatu na mia ine za feza, toni elfu moja za ngano na kilo elfu moja za shayiri, waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.