2 Chronicles 28:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahazi alianza kutawala akiwa na umri wa miaka ishirini; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita huko Yerusalemu. Yeye, hakufuata mfano mzuri wa Daudi babu yake, bali alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, kama Daudi babaye;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ahazi alianza kutawala akiwa na umri wa miaka ishirini; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita huko Yerusalemu. Yeye, hakufuata mfano mzuri wa Daudi babu yake, bali alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama Daudi babaye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahazi alianza kutawala akiwa na umri wa miaka ishirini; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita huko Yerusalemu. Yeye, hakufuata mfano mzuri wa Daudi babu yake, bali alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahazi alikuwa mwenye miaka 20 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 16 mle Yerusalemu; hakuyafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama baba yake Dawidi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama Daudi babaye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahazi alianza kutawala akiwa na umri wa miaka makumi mbili, alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita kule Yerusalema. Yeye, hakufuata mufano muzuri wa Daudi babu yake, lakini alitenda maovu mbele za Yawe,