2 Chronicles 28:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa mnanuia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Je, hamtambui ya kuwa nyinyi pia mmetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi sasa mnakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Lakini ninyi je, hamna pia hatia ya dhambi mliyotenda dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa mwanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu, wawe kwenu watumwa na wajakazi; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya Bwana, Mungu wenu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa mnanuia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Je, hamtambui ya kuwa nyinyi pia mmetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi sasa mnakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Lakini ninyi je, hamna pia hatia ya dhambi mliyotenda dhidi ya BWANA Mungu wenu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi sasa mnakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Lakini ninyi je, hamna pia hatia ya dhambi mliyotenda dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wenu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa mnanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu na kuwafanya wawe watumwa na wajakazi wenu; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya BWANA, Mungu wenu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa mnanuia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Je, hamtambui ya kuwa nyinyi pia mmetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa ninyi mwataka kuwanyenyekeza kwa nguvu hawa wana wa Yuda na wa Yerusalemu, wawe watumwa na vijakazi wenu. Lakini nanyi mliyojipatia kwake Bwana Mungu wenu sizo manza tu, mlizozikora?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa mwanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu, wawe kwenu watumwa na wajakazi; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya BWANA, Mungu wenu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa munakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalema watumwa wenu. Hamutambui kwamba ninyi vilevile mumetenda zambi mbele ya Yawe, Mungu wenu?