2 Chronicles 28:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakawaambia, “Msiwalete humu mateka hao, kwa sababu mnanuia kutuletea hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu; tendo hili huku litakuwa nyongeza ya dhambi yetu na hatia yetu; kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa na kuna ghadhabu kali juu ya Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwambia, “Hamna ruhusa kuwaleta hao wafungwa hapa, ama sivyo tutakuwa na hatia mbele za Mwenyezi Mungu. Je, mnataka kuongezea dhambi yetu na hatia yetu? Kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa, nayo hasira kali ya Mwenyezi Mungu iko juu ya Israeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za Bwana, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakawaambia, “Msiwalete humu mateka hao, kwa sababu mnanuia kutuletea hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu; tendo hili huku litakuwa nyongeza ya dhambi yetu na hatia yetu; kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa na kuna ghadhabu kali juu ya Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwambia, “Hamna ruhusa kuwaleta hao wafungwa hapa, ama sivyo tutakuwa na hatia mbele za BWANA. Je, mnataka kuongezea dhambi yetu na hatia yetu? Kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa, nayo hasira kali ya BWANA iko juu ya Israeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwambia, “Hamna ruhusa kuwaleta hao wafungwa hapa, ama sivyo tutakuwa na hatia mbele za bwana. Je, mnataka kuongezea dhambi yetu na hatia yetu? Kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa, nayo hasira kali ya bwana iko juu ya Israeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za BWANA, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakawaambia, “Msiwalete humu mateka hao, kwa sababu mnanuia kutuletea hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu; tendo hili huku litakuwa nyongeza ya dhambi yetu na hatia yetu; kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa na kuna ghadhabu kali juu ya Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakawaambia: Msiyalete mateka yenu hapa! Kwani hivyo tutakora manza kwa Bwana, nanyi mnataka kweli kuyaongeza makosa yetu na manza zetu, kwani manza zetu ni nyingi, nayo makali yawakayo moto yanatukalia sisi Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za BWANA, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakawaambia: “Musiwalete humu wafungwa hao, kwa sababu munakusudia kutuletea kosa mbele ya Yawe, tendo hili huku litakuwa nyongezo ya zambi yetu na kosa letu; kwa sababu kosa letu tayari ni kubwa na kuna kasirani kali juu ya Israeli.”