2 Chronicles 28:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huohuo pia, Wafilisti walikuwa wakiishambulia miji ya Shefela na Negebu ya Yuda. Waliiteka miji ya Beth-shemeshi, Ayaloni, Gederothi, Soko na vijiji vyake, Timna na vijiji vyake, Gimzo na vijiji vyake, wakafanya makao yao huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Wafilisti walikuwa wameshambulia miji iliyokuwa chini ya vilima na katika miji ya Negebu ya Yuda. Wakatwaa Beth-Shemeshi, Aiyaloni, Gederothi, Soko pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake, Gimzo pia pamoja na vijiji vyake, wakaishi humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wafilisti pia walikuwa wameingia miji ya Shefela, na ya Negebu ya Yuda, nao wameutwaa Beth-shemeshi, na Ayaloni, na Gederothi, na Soko pamoja na miji yake, na Timna pamoja na miji yake, na Gimzo pia na miji yake; wakakaa humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huohuo pia, Wafilisti walikuwa wakiishambulia miji ya Shefela na Negebu ya Yuda. Waliiteka miji ya Beth-shemeshi, Ayaloni, Gederothi, Soko na vijiji vyake, Timna na vijiji vyake, Gimzo na vijiji vyake, wakafanya makao yao huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Wafilisti walikuwa wameshambulia miji iliyokuwa chini ya vilima na katika miji ya Negebu ya Yuda. Nao wakawa wametwaa Beth-Shemeshi, Aiyaloni, Gederothi, Soko pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake, Gimzo pia pamoja na vijiji vyake na kuishi humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Wafilisti walikuwa wameshambulia miji iliyokuwa chini ya vilima na katika miji ya Negebu ya Yuda. Nao wakawa wametwaa Beth-Shemeshi, Aiyaloni, Gederothi, Soko pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake, Gimzo pia pamoja na vijiji vyake na kuishi humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wafilisti pia walikuwa wameishambulia na kuitwaa miji ya Shemeshi, Ayaloni, Gederothi, soko, pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake na Gimzo pia na vijiji vyake, miji yake; wakakaa humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huohuo pia, Wafilisti walikuwa wakiishambulia miji ya Shefela na Negebu ya Yuda. Waliiteka miji ya Beth-shemeshi, Ayaloni, Gederothi, Soko na vijiji vyake, Timna na vijiji vyake, Gimzo na vijiji vyake, wakafanya makao yao huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Wafilisti wakaiingia miji ya nchi ya tambarare na miji ya kusini katika nchi ya Yuda na kunyang'anya mali, wakateka Beti-Semesi na Ayaloni na Gederoti na Soko na mitaa yake na Timuna na mitaa yake na Gimuzo na mitaa yake, wakakaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wafilisti pia walikuwa wameingia miji ya Shefela, na ya Negebu ya Yuda, nao wameutwaa Beth-shemeshi, na Ayaloni, na Gederothi, na Soko pamoja na miji yake, na Timna pamoja na miji yake, na Gimzo pia na miji yake; wakakaa humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati uleule, Wafilistini walikuwa wakiishambulia miji ya Sefela na Negebu ya Yuda. Walinyanganya miji ya Beti-Semesi, Ayaloni, Gederoti, Soko na vijiji vyake, Timuna na vijiji vyake, Gimuzo na vijiji vyake, wakafanya makao yao kule.