2 Chronicles 28:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu mfalme Ahazi wa Israeli alikuwa na ukatili kwa watu wake, na alikosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu aliwafanya watu wa Yuda wakose nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu aliishusha Yuda kwa sababu ya Ahazi mfalme wa Israeli, kwa kuwa alikuwa ameongeza uovu katika Yuda na kumkosea Mwenyezi Mungu mno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi Bwana mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu mfalme Ahazi wa Israeli alikuwa na ukatili kwa watu wake, na alikosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu aliwafanya watu wa Yuda wakose nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA aliishusha Yuda kwa sababu ya Ahazi mfalme wa Israeli, kwa kuwa alikuwa ameongeza uovu katika Yuda na kumkosea BWANA mno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana aliishusha Yuda kwa sababu ya Ahazi mfalme wa Israeli, kwa kuwa alikuwa ameongeza uovu katika Yuda na kumkosea bwana mno.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana BWANA aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi BWANA mno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu mfalme Ahazi wa Israeli alikuwa na ukatili kwa watu wake, na alikosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu aliwafanya watu wa Yuda wakose nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana aliwanyenyekeza Wayuda kwa ajili ya Ahazi, mfalme wa Waisiraeli, kwani aliwalegeza Wayuda alipomvunjia Bwana maagano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana BWANA aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi BWANA mno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Yawe alinyenyekeza inchi ya Yuda kwa ajili ya Ahazia mufalme wa Israeli sababu yeye alifanya uasherati katika Yuda na kumwasi Yawe.