2 Chronicles 28:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akafukiza ubani kwenye Bonde la mwana wa Hinomu na kuwateketeza wanawe kama tambiko, akiiga desturi za kuchukiza za watu ambao walifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Ben-Hinomu, na kuwatoa kafara watoto wake kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa Mwenyezi Mungu aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akafukiza ubani kwenye Bonde la mwana wa Hinomu na kuwateketeza wanawe kama tambiko, akiiga desturi za kuchukiza za watu ambao walifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Hinomu na kuwatoa wanawe kafara kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa BWANA aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Ben-Hinomu, na kuwatoa wanawe kafara kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa bwana aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akafukiza ubani kwenye Bonde la mwana wa Hinomu na kuwateketeza wanawe kama tambiko, akiiga desturi za kuchukiza za watu ambao walifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye yeye akavukiza bondone kwa Bin-Hinomu, hata wanawe akawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni akiyafuata hayo matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akafukiza ubani kwenye Bonde la mwana wa Hinomu na kuwateketeza wana wake kama sadaka, akiiga desturi za kuchukiza za watu ambao walifukuzwa na Yawe wakati Waisraeli walipokuwa wanaingia katika inchi.