2 Chronicles 28:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliua askari mashujaa wa Yuda 120,000 katika siku moja. Ilitokea hivyo kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari elfu mia moja na ishirini katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu mia na ishirini elfu, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliua askari mashujaa wa Yuda 120,000 katika siku moja. Ilitokea hivyo kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari 120,000 katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari 120,000 katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu elfu mia moja na ishirini, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliua askari mashujaa wa Yuda 120,000 katika siku moja. Ilitokea hivyo kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Peka, mwana wa Remalia, akaua katika nchi ya Yuda siku moja watu 120000, wote walikuwa wenye nguvu, kwa kuwa walimwacha Bwana Mungu wa baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu mia na ishirini elfu, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Peka, mwana wa Remalia akawaua watu wengi sana. Aliua waaskari mashujaa wa Yuda elfu mia moja na makumi mbili katika siku moja. Ilitokea vile kwa sababu walimwacha Yawe, Mungu wa babu zao.