2 Chronicles 28:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jeshi la Israeli lilichukua mateka ndugu zao watu laki mbili wakiwemo wanawake na watoto. Waliwachukua hadi Samaria pamoja na mali nyingi waliyoteka nyara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakawachukua mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao elfu mia mbili, wakiwa wanawake, pamoja na watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakachukua wa ndugu zao wafungwa mia mbili elfu, wanawake, na wana, na binti, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jeshi la Israeli lilichukua mateka ndugu zao watu laki mbili wakiwemo wanawake na watoto. Waliwachukua hadi Samaria pamoja na mali nyingi waliyoteka nyara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakawachukuwa mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao 200,000 hawa wakiwa ni wanawake, watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakawachukua mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao 200,000 hawa wakiwa ni wanawake, watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waisraeli wakachukua mateka ndugu zao wafungwa elfu mia mbili wakiwemo wanawake, watoto wa kiume na kike, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jeshi la Israeli lilichukua mateka ndugu zao watu laki mbili wakiwemo wanawake na watoto. Waliwachukua hadi Samaria pamoja na mali nyingi waliyoteka nyara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Isiraeli wakateka kwa ndugu zao 200000, wanawake na watoto wa kiume na wa kike na mali nyingi, walizozinyang'anya kwao; haya mateka wakayapeleka Samaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakachukua wa ndugu zao wafungwa mia mbili elfu, wanawake, na wana, na binti, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jeshi la Israeli likapeleka wafungwa wandugu zao watu elfu mia mbili, wanawake na watoto. Waliwapeleka mpaka Samaria pamoja na mali nyingi waliyonyanganya.