2 Chronicles 29:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hezekia alianza kutawala Yuda akiwa na umri wa miaka ishirini na mitano, akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka ishirini na tisa. Mama yake alikuwa Abiya binti Zekaria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hezekia alianza kutawala Yuda akiwa na umri wa miaka ishirini na mitano, akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka ishirini na tisa. Mama yake alikuwa Abiya binti Zekaria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hezekia alianza kutawala Yuda akiwa na umri wa miaka ishirini na mitano, akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka ishirini na tisa. Mama yake alikuwa Abiya binti Zekaria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia akaupata ufalme alipokuwa mwenye miaka 25, akawa mfalme miaka 29 mle Yerusalemu. Jina la mama yake ni Abia, binti Zakaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia alianza kutawala Yuda akiwa na umri wa miaka makumi mbili na mitano, akatawala kule Yerusalema kwa muda wa miaka makumi mbili na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti ya Zakaria.