2 Chronicles 29:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi wanangu, muwe na nidhamu. Mwenyezi-Mungu amewachagua nyinyi ili mumtumikie, muwaongoze watu wake katika ibada, na kumfukizia ubani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wanangu, msijipurukushe sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi wanangu, muwe na nidhamu. Mwenyezi-Mungu amewachagua nyinyi ili mumtumikie, muwaongoze watu wake katika ibada, na kumfukizia ubani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa bwana amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wanangu, msiyapuuze haya, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi wanangu, muwe na nidhamu. Mwenyezi-Mungu amewachagua nyinyi ili mumtumikie, muwaongoze watu wake katika ibada, na kumfukizia ubani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa ninyi wanangu, msizurure! Kwani ninyi Bwana aliwachagua, msimame mbele yake na kumtumikia, mwe watumishi wake na wavukizaji wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wanangu, msijipurukushe sasa, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wana wangu, musikuwe wavivu. Yawe amewachagua ninyi kusudi mumutumikie, muwaongoze watu wake katika ibada, na kumufukizia ubani.”