2 Chronicles 29:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani waliingia katika sehemu ya ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakautoa uchafu wote uliokuwemo, wakauweka uani. Kutoka hapo, Walawi waliuchukua uchafu huo mpaka nje kwenye Bonde la Kidroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao makuhani wakaingia nyumbani mwa Bwana, katika mahali pa ndani, ili waisafishe, wakatoa uchafu wote waliouona hekaluni mwa Bwana, wakautupa nje uani mwa nyumba ya Bwana. Walawi wakautwaa, ili wauchukue nje mpaka kijito cha Kidroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani waliingia katika sehemu ya ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakautoa uchafu wote uliokuwemo, wakauweka uani. Kutoka hapo, Walawi waliuchukua uchafu huo mpaka nje kwenye Bonde la Kidroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la BWANA ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la BWANA. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la bwana ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la bwana. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao makuhani wakaingia nyumbani mwa BWANA, katika mahali pa ndani, ili waisafishe, wakatoa uchafu wote waliouona hekaluni mwa BWANA, wakautupa nje uani mwa nyumba ya BWANA. Walawi wakautwaa, ili wauchukue nje mpaka kijito cha Kidroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani waliingia katika sehemu ya ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakautoa uchafu wote uliokuwemo, wakauweka uani. Kutoka hapo, Walawi waliuchukua uchafu huo mpaka nje kwenye Bonde la Kidroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji wakaingia Nyumbani mwa Bwana ndani kuitakasa na kuyatoa machafu yote, waliyoyaona Jumbani mwa Bwana, wakayapeleka uani penye Nyumba ya Bwana; ndiko, Walawi walikoyachukua, wayapeleke nje mtoni kwa Kidoroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao makuhani wakaingia nyumbani mwa BWANA, katika mahali pa ndani, ili waisafishe, wakatoa uchafu wote waliouona hekaluni mwa BWANA, wakautupa nje uani mwa nyumba ya BWANA. Walawi wakautwaa, ili wauchukue nje mpaka kijito cha Kidroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani wakaingia katika sehemu ya ndani ya nyumba ya Yawe, wakatosha uchafu wote uliokuwa mule, wakauweka katika kiwanja. Kutoka pale, Walawi walitwaa uchafu ule mpaka inje kwenye Bonde la Kidroni.