2 Chronicles 29:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walianza kazi ya kulitakasa hekalu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, na kufikia siku ya nane, wakawa wamekwisha maliza kazi yote, hata na ukumbini. Kisha, walifanya kazi kwa muda wa siku nane zaidi hadi siku ya kumi na sita ya mwezi huo, kila kitu kilikamilika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa Mwenyezi Mungu. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lenyewe, wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakaanza kutakasa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika ukumbi wa Bwana; wakaitakasa nyumba ya Bwana katika muda wa siku nane; wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walianza kazi ya kulitakasa hekalu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, na kufikia siku ya nane, wakawa wamekwisha maliza kazi yote, hata na ukumbini. Kisha, walifanya kazi kwa muda wa siku nane zaidi hadi siku ya kumi na sita ya mwezi huo, kila kitu kilikamilika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa BWANA. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu lenyewe la BWANA wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa bwana. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu lenyewe la bwana wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakaanza kutakasa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika ukumbi wa BWANA; wakaitakasa nyumba ya BWANA katika muda wa siku nane; wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walianza kazi ya kulitakasa hekalu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, na kufikia siku ya nane, wakawa wamekwisha maliza kazi yote, hata na ukumbini. Kisha, walifanya kazi kwa muda wa siku nane zaidi hadi siku ya kumi na sita ya mwezi huo, kila kitu kilikamilika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakaanza kuitakasa, siku ya nane ya huo mwezi wakafika penye ukumbi wa Bwana, wakaitakasa Nyumba ya Bwana tena siku nane, wakaimaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakaanza kutakasa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika ukumbi wa BWANA; wakaitakasa nyumba ya BWANA katika muda wa siku nane; wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walianza kazi ya kutakasa hekalu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, na kufikia siku ya nane, wakakuwa wamekwisha kumaliza kazi yote, hata na baraza. Kisha, wakafanya kazi kwa muda wa siku nane zaidi mpaka siku ya kumi na sita ya mwezi ule, kila kitu kikakamilika.