2 Chronicles 29:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, Walawi walimwendea mfalme Hezekia wakamwambia, “Tumekwisha litakasa hekalu lote pamoja na madhabahu ya tambiko za kuteketeza na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate mitakatifu na vyombo vyake vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lote, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaingia ndani kwa Hezekia mfalme, wakasema, Tumeisafisha nyumba yote ya Bwana, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate ya wonyesho, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, Walawi walimwendea mfalme Hezekia wakamwambia, “Tumekwisha litakasa hekalu lote pamoja na madhabahu ya tambiko za kuteketeza na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate mitakatifu na vyombo vyake vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu lote la BWANA, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu lote la bwana, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaingia ndani kwa Hezekia mfalme, wakasema, Tumeisafisha nyumba yote ya BWANA, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate ya wonyesho, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, Walawi walimwendea mfalme Hezekia wakamwambia, “Tumekwisha litakasa hekalu lote pamoja na madhabahu ya tambiko za kuteketeza na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate mitakatifu na vyombo vyake vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakaingia nyumbani kwa mfalme Hizikia, wakamwamiba: Tumeitakasa Nyumba yote ya Bwana, hata meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko na vyombo vyake vyote,, hata meza ya mikate, aliyowekewa Bwana, na vyombo vyake vyote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaingia ndani kwa Hezekia mfalme, wakasema, Tumeisafisha nyumba yote ya BWANA, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate ya wonyesho, pamoja na vyombo vyake vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Walawi wakamwendea mufalme Hezekia wakamwambia: “Tumekwisha kutakasa hekalu lote pamoja na mazabahu ya sadaka za kuteketeza kwa moto na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate inayotolewa kwa Mungu na vyombo vyake vyote.