2 Chronicles 29:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, vyombo vyote ambavyo mfalme Ahazi alivyoviondoa wakati wa utawala wake, hapo alipoasi, tumevirudisha na kuviweka wakfu. Vyote vipo mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena vyombo vyote alivyovitupa mfalme Ahazi alipotawala, hapo alipoasi, tumevitengeza na kuvitakasa; navyo, tazama, vipo mbele ya madhabahu ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, vyombo vyote ambavyo mfalme Ahazi alivyoviondoa wakati wa utawala wake, hapo alipoasi, tumevirudisha na kuviweka wakfu. Vyote vipo mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote vile ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa wakati alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote vile ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa wakati alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena vyombo vyote alivyovitupa mfalme Ahazi alipotawala, hapo alipoasi, tumevitengeza na kuvitakasa; navyo, tazama, vipo mbele ya madhabahu ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, vyombo vyote ambavyo mfalme Ahazi alivyoviondoa wakati wa utawala wake, hapo alipoasi, tumevirudisha na kuviweka wakfu. Vyote vipo mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyombo vyote, mfalme Ahazi alivyovichafua katika ufalme wake, alipoyavunja maagano, tumevitengeneza na kuvitakasa, utaviona, viko mbele ya meza ya kumtambikia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena vyombo vyote alivyovitupa mfalme Ahazi alipotawala, hapo alipoasi, tumevitengeza na kuvitakasa; navyo, tazama, vipo mbele ya madhabahu ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, tumerudisha na kutakasa vyombo vyote ambavyo mufalme Ahazi alivyotupa wakati wa utawala wake, pale alipoasi. Vyote vipo mbele ya mazabahu ya Yawe.”