2 Chronicles 29:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakaleta mafahali saba, kondoo madume saba, wanakondoo saba na mbuzi madume saba, wawe sadaka ya kuondoa dhambi, kwa ajili ya jamaa ya kifalme, patakatifu na watu wa Yuda. Hapo, mfalme aliwaambia makuhani waliokuwa wazawa wa Aroni wawateketeze juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na beberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Haruni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaleta ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba, na wana-kondoo saba, na mabeberu saba, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, na kwa ajili ya patakatifu, na kwa ajili ya Yuda. Akaamuru makuhani, wana wa Haruni, wawatoe madhabahuni pa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakaleta mafahali saba, kondoo madume saba, wanakondoo saba na mbuzi madume saba, wawe sadaka ya kuondoa dhambi, kwa ajili ya jamaa ya kifalme, patakatifu na watu wa Yuda. Hapo, mfalme aliwaambia makuhani waliokuwa wazawa wa Aroni wawateketeze juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaleta mafahali saba, kondoo waume saba, wana-kondoo waume saba na mabeberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Aroni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na mabeberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Haruni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaleta ng'ombe dume saba, na kondoo dume saba, na wana-kondoo saba, na mabeberu saba, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, na kwa ajili ya patakatifu, na kwa ajili ya Yuda. Akaamuru makuhani, wana wa Haruni, wawatoe madhabahuni pa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakaleta mafahali saba, kondoo madume saba, wanakondoo saba na mbuzi madume saba, wawe sadaka ya kuondoa dhambi, kwa ajili ya jamaa ya kifalme, patakatifu na watu wa Yuda. Hapo, mfalme aliwaambia makuhani waliokuwa wazawa wa Aroni wawateketeze juu ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaleta madume saba ya ng'ombe na madume saba ya kondoo na wana kondoo saba na madume saba ya mbuzi kuwa ng'ombe za tambiko za weuo kwa ajili ya ufalme na kwa ajili ya Patakatifu na kwa ajili ya Wayuda. Akawaambia watambikaji, wana wa Haroni, wawatoe kuwa ng'ombe za tambiko hapo pa kumtambikia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaleta ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, na wana-kondoo saba, na mabeberu saba, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, na kwa ajili ya patakatifu, na kwa ajili ya Yuda. Akaamuru makuhani, wana wa Haruni, wawatoe madhabahuni pa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaleta ngombe dume saba, kondoo dume saba, wana-kondoo saba na mbuzi dume saba, kuwa sadaka ya maondoleo ya zambi, kwa ajili ya jamaa ya kifalme, ya Pahali Patakatifu na ya watu wa Yuda. Kwa hiyo, mufalme akawaambia makuhani waliokuwa wazao wa Haruni wawateketeze juu ya mazabahu ya Yawe.