2 Chronicles 29:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo waume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo waume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo waume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo dume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipowachinja hao ng'ombe, nao watambikaji wakazichukua damu zao, wakazinyunyizia meza ya kutambikia; wakawachinja nao madume ya kondoo, nazo damu zao wakazinyunyizia meza ya kutambikia, wakawachinja nao wana kondoo, nazo damu zao wakazinyunyizia meza ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakawachinja ng’ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo waume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani walichinja ngombe dume kwanza, kisha kondoo dume, halafu wana-kondoo na kila mara walitwaa damu ya nyama wale na kuinyunyiza juu ya mazabahu.