2 Chronicles 29:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Hezekia aliyafuata maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amempa mfalme Daudi kwa njia ya Gadi mwonaji wa mfalme na nabii Nathani. Hivyo basi, akaweka Walawi katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baadhi yao wakiwa na matoazi, wengine vinanda na wengine vinubi. Hiyo ilikuwa amri ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya manabii wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na Mwenyezi Mungu kupitia manabii wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Hezekia aliyafuata maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amempa mfalme Daudi kwa njia ya Gadi mwonaji wa mfalme na nabii Nathani. Hivyo basi, akaweka Walawi katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baadhi yao wakiwa na matoazi, wengine vinanda na wengine vinubi. Hiyo ilikuwa amri ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya manabii wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la BWANA wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamuriwa na BWANA kupitia manabii wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la bwana wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na bwana kupitia manabii wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Hezekia aliyafuata maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amempa mfalme Daudi kwa njia ya Gadi mwonaji wa mfalme na nabii Nathani. Hivyo basi, akaweka Walawi katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baadhi yao wakiwa na matoazi, wengine vinanda na wengine vinubi. Hiyo ilikuwa amri ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya manabii wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alikuwa amewasimamisha Walawi penye Nyumba ya Bwana, wakiyashika matoazi na mapango na mazeze, kama Dawidi na Gadi aliyekuwa mchunguzaji wa mfalme na mfumbuaji Natani walivyoviagiza; kwani agizo hilo lilitoka kwa Bwana, likatokea vinywani mwa wafumbuaji wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Hezekia alifuata maagizo ambayo Yawe alikuwa amemupa mufalme Daudi kwa njia ya Gadi, nabii wa mufalme na nabii Natani. Hivyo basi, akaweka Walawi katika nyumba ya Yawe, wamoja wao wakiwa na matoazi, wengine vinanda na wengine vinubi. Hiyo ilikuwa amri ya Yawe kwa njia ya manabii wake.