2 Chronicles 29:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hezekia akaamuru sadaka ya kuteketeza itolewe juu ya madhabahu. Mara tu tambiko hiyo ilipoanza kutolewa, watu walianza kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo zilizoandamana na mlio wa tarumbeta na vyombo vya muziki vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia Mwenyezi Mungu pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa Bwana, na mapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hezekia akaamuru sadaka ya kuteketeza itolewe juu ya madhabahu. Mara tu tambiko hiyo ilipoanza kutolewa, watu walianza kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo zilizoandamana na mlio wa tarumbeta na vyombo vya muziki vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia BWANA pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia bwana pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa BWANA, na parapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Hezekia akaamuru sadaka ya kuteketeza itolewe juu ya madhabahu. Mara tu tambiko hiyo ilipoanza kutolewa, watu walianza kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo zilizoandamana na mlio wa tarumbeta na vyombo vya muziki vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia alipoagiza kuziteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa kutambikia, papo hapo tambiko lilipanzia, ndipo, wimbo wa Bwana ulipoanzia pamoja na matarumbeta yaliyoongozwa na vyombo vya Dawidi, mfalme wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa BWANA, na mapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hezekia akaamuru sadaka ya kuteketeza kwa moto itolewe juu ya mazabahu. Mara tu sadaka hiyo ilipoanza kutolewa, watu wakaanza kumusifu Yawe kwa nyimbo zilizofuatana na mulio wa baragumu na vyombo vya muziki vya Daudi, mufalme wa Israeli.