2 Chronicles 29:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme Hezekia na viongozi wakawaambia Walawi wamsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo alizotunga mfalme Daudi na mwonaji Asafu. Basi, watu wote wakamtukuza Mungu kwa furaha, na kumsujudia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu Mwenyezi Mungu kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha, nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme Hezekia na viongozi wakawaambia Walawi wamsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo alizotunga mfalme Daudi na mwonaji Asafu. Basi, watu wote wakamtukuza Mungu kwa furaha, na kumsujudia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu BWANA kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu bwana kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme Hezekia na viongozi wakawaambia Walawi wamsifu Mwenyezi-Mungu kwa nyimbo alizotunga mfalme Daudi na mwonaji Asafu. Basi, watu wote wakamtukuza Mungu kwa furaha, na kumsujudia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Hizikia na wakuu wakawaambia Walawi, wamtukuze Bwana na kuyaimba maneno ya Dawidi na ya mchunguzaji Asafu. Ndipo, walipomtukuza kwa furaha, kisha wakainama, wakamwangukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme Hezekia na viongozi wakawaambia Walawi wamusifu Yawe kwa nyimbo ambazo mufalme Daudi na nabii Asafu walizotunga. Basi, watu wote wakamutukuza Mungu kwa furaha, na kuinama uso mpaka chini.