2 Chronicles 29:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Hezekia akawaambia watu, “Maadamu sasa mmekwisha jitakasa, karibieni, leteni sadaka na matoleo ya shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Basi, watu wakaleta sadaka zao na matoleo yao ya shukrani, na tambiko za kuteketeza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu. Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa Mwenyezi Mungu.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa Bwana, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa Bwana. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Hezekia akawaambia watu, “Maadamu sasa mmekwisha jitakasa, karibieni, leteni sadaka na matoleo ya shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Basi, watu wakaleta sadaka zao na matoleo yao ya shukrani, na tambiko za kuteketeza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa BWANA. Njoni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa BWANA.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa bwana. Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa bwana.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko lote likaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Hezekia akawaambia watu, “Maadamu sasa mmekwisha jitakasa, karibieni, leteni sadaka na matoleo ya shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Basi, watu wakaleta sadaka zao na matoleo yao ya shukrani, na tambiko za kuteketeza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hizikia akawaitikia akisema: Sasa mmeyajaza magao yenu kumtumikia Bwana, basi, karibuni, mlete huku kwenye Nyumba ya Bwana ng'ombe za tambiko na vipaji vya shukrani! Ndipo, watu wa huo mkutano walipoleta ng'ombe za tambiko na vipaji vya shukrani, kila mtu akatoa ng'ombe za tambiko, kama moyo ulivyopenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Hezekia akawaambia watu: “Sasa mumekwisha kujitakasa, mukaribie, mulete sadaka na matoleo ya shukrani katika nyumba ya Yawe.” Basi, watu wakaleta sadaka zao na matoleo yao ya shukrani, na za kuteketeza.