2 Chronicles 29:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo dume mia mbili. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa walizozileta kusanyiko ikawa ng'ombe waume sabini, kondoo waume mia, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo waume 100 na wana-kondoo waume 200. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume 100 na wana-kondoo dume 200. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa mkutano walizozileta ni ng'ombe dume sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hesabu ya ng'ombe za tambiko, watu wa huo mkutano walizozitoa, ikawa ng'ombe 70, madume ya kondoo 100, wana kondoo 200; hawa wote walikuwa wa kumteketezea Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa walizozileta kusanyiko ikawa ng’ombe waume sabini, kondoo waume mia, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sadaka za kuteketeza walizoleta kwa jumla zilikuwa ngombe dume makumi saba, kondoo dume mia moja na wana-kondoo mia mbili. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa ajili ya Yawe.