2 Chronicles 29:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana babu zetu waliasi na kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Wamemwacha, wakageuzia mbali nyuso zao na kupawekea kisogo mahali aishipo Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Mwenyezi Mungu wakamgeuzia visogo vyao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana baba zetu wameasi, na kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wetu, wamemwacha, na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya Bwana, na kumpa maungo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana babu zetu waliasi na kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Wamemwacha, wakageuzia mbali nyuso zao na kupawekea kisogo mahali aishipo Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa BWANA Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya BWANA wakamgeuzia visogo vyao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa bwana Mwenyezi Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya bwana wakamgeuzia visogo vyao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana baba zetu wameasi, na kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, Mungu wetu, wamemwacha, na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya BWANA, na kumpa mgongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana babu zetu waliasi na kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Wamemwacha, wakageuzia mbali nyuso zao na kupawekea kisogo mahali aishipo Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani baba zetu wameyavunja maagano, wakayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wetu, wakamwacha na kuzigeuza nyuso zao, zisilitazame Kao la Bwana, wakalielekezea migongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana baba zetu wameasi, na kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, Mungu wetu, wamemwacha, na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya BWANA, na kumpa maungo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana babu zetu waliasi na kutenda maovu mbele ya Yawe, Mungu wetu. Wamemwacha na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya Yawe.