2 Chronicles 29:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, waliifunga milango ya ukumbi, wakazizima taa, na hawajafukiza ubani wala kutoa tambiko za kuteketeza katika mahali patakatifu pa Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, waliifunga milango ya ukumbi, wakazizima taa, na hawajafukiza ubani wala kutoa tambiko za kuteketeza katika mahali patakatifu pa Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yo yote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, waliifunga milango ya ukumbi, wakazizima taa, na hawajafukiza ubani wala kutoa tambiko za kuteketeza katika mahali patakatifu pa Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaifunga nayo milango ya ukumbi, wakazizima taa zake, hawakumvukizia Mungu wa Isiraeli mavukizo, wala hawakumtolea ng'ombe za tambiko hapa Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, wamefunga milango ya baraza, wakazimisha taa, na hawajafukiza ubani wala kutoa sadaka za kuteketeza kwa moto katika Pahali Patakatifu pa Mungu wa Israeli.