2 Chronicles 3:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu; bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mabawa ya haya Makerubi urefu wao ulikuwa mikono 20: bawa la moja lenye mikono mitano liligusa ukuta wa nyumba, nalo la pili lenye mikono mitano liligusa bawa la Kerubi la pili;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila kerubi ilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa metre ine na nusu kwa jumla, metre mbili na sentimetre makumi mbili na tano kila bawa. Bawa moja liligusa ukuta upande mumoja wa chumba na la pili liligusana na la kerubi wa pili.