2 Chronicles 3:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Solomoni alitengeneza nguzo mbili za shaba, kila moja yenye urefu wa mita 15.5, akaziweka mbele ya nyumba. Kila nguzo ilikuwa na taji juu yake yenye urefu wa mita 2.2.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbele ya Hekalu Sulemani akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na urefu wa dhiraa thelathini na tano kwenda juu, na kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye kimo cha dhiraa tano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Solomoni alitengeneza nguzo mbili za shaba, kila moja yenye urefu wa mita 15.5, akaziweka mbele ya nyumba. Kila nguzo ilikuwa na taji juu yake yenye urefu wa mita 2.2.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbele ya Hekalu Solomoni akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbele ya Hekalu Sulemani akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake, na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na mataji yaliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Solomoni alitengeneza nguzo mbili za shaba, kila moja yenye urefu wa mita 15.5, akaziweka mbele ya nyumba. Kila nguzo ilikuwa na taji juu yake yenye urefu wa mita 2.2.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbele ya nyumba akaweka nguzo mbili zenye urefu wa mikono 35, nacho kichwa kilichokuwa juu ya kila moja kilikuwa chenye urefu wa mikono mitano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Solomono alitengeneza nguzo mbili za shaba, kila moja yenye urefu wa metre mia moja kumi na tano na nusu, akaziweka mbele ya nyumba. Kisha akatengeneza taji mbili, kila moja yenye urefu wa metre mbili na sentimetre makumi mbili na tano, akaziweka juu ya nguzo zile.