2 Chronicles 3:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alizisimamisha nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu, moja upande wa kusini, na nyingine upande wa kaskazini; ile ya upande wa kusini aliita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alizisimamisha nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu, moja upande wa kusini, na nyingine upande wa kaskazini; ile ya upande wa kusini aliita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kulia, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kulia Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alizisimamisha nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu, moja upande wa kusini, na nyingine upande wa kaskazini; ile ya upande wa kusini aliita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya jumba hili, moja kuumeni, moja kushotoni; ya kuumeni akaiita Yakini (Hushikiza), ya kushotoni Boazi (Nguvu imo).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akazisimamisha nguzo zile kwenye baraza ya hekalu, moja upande wa kusini, na ingine upande wa kaskazini; ile ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.