2 Chronicles 3:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo, na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake ulikuwa sawa na upana wa nyumba ulikuwa dhiraa ishirini, na kimo chake mia moja na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukumbi uliokuwa mbele ya nyumba ulikuwa mikono 20 kwa kuupatanisha na upana wa nyumba, nao urefu wa kwenda juu ulikuwa mikono 120, ndani akazifunika kuta zake kwa mabati ya dhahabu tupu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa metre kenda, sawa na upana wa nyumba hiyo, na urefu kwenda juu metre makumi tano na ine. Kuta zake zilifunikwa kwa zahabu safi upande wa ndani.