2 Chronicles 3:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukumbi ulizungushiwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuchorwa mifano ya miti ya mitende na minyororo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za msunobari, na kufunikwa kwa dhahabu safi, na kuupamba kwa michoro ya mitende na minyororo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukumbi ulizungushiwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuchorwa mifano ya miti ya mitende na minyororo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo nyumba kubwa ilizungushiwa miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, juu yake akaichora mitende na minyororo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukumbi ulizungushiwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuchorwa mifano ya miti ya mitende na minyororo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyumba kubwa akaipigilia kutani mbao za mivinje, nazo akazivika mabati ya dhahabu nzuri, humo namo akachora mitende na mikufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baraza ilifunikwa kwa mbao za miberoshi. Kisha kwa zahabu safi na kuchorwa mifano ya miti ya ngazi na minyororo.