2 Chronicles 3:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, alipatengeneza mahali patakatifu sana. Urefu wake ulikuwa mita 9, sawasawa na upana wake ambao pia ulikuwa mita 9. Alitumia zaidi ya tani 20 za dhahabu kukifunika chumba hicho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 600 za dhahabu safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, alipatengeneza mahali patakatifu sana. Urefu wake ulikuwa mita 9, sawasawa na upana wake ambao pia ulikuwa mita 9. Alitumia zaidi ya tani 20 za dhahabu kukifunika chumba hicho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120 za dhahabu safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120 za dhahabu safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake sawa na upana wa nyumba, ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, alipatengeneza mahali patakatifu sana. Urefu wake ulikuwa mita 9, sawasawa na upana wake ambao pia ulikuwa mita 9. Alitumia zaidi ya tani 20 za dhahabu kukifunika chumba hicho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akapatengeneza Patakatifu Penyewe, urefu wake ulikuwa mikono 20 kwa kuupatanisha na upana wa nyumba, upana wake nao ulikuwa mikono 20, akapavika mabati ya dhahabu nzuri za vipande vya dhahabu 600, ndio frasila 1800.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, alipatengeneza Pahali Patakatifu Sana. Urefu wake ulikuwa metre kenda, sawasawa na upana wake ambao vilevile ulikuwa metre tisa. Alitumia zaidi ya toni makumi mbili za zahabu kwa kupakaa ndani ya chumba kile.