2 Chronicles 30:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Hezekia aliwatumia ujumbe watu wote wa Israeli na Yuda, na pia akawaandikia barua wenyeji wa Efraimu na Manase, akiwaalika wote waje katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu Yerusalemu, ili kuiadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa heshima yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akatuma ujumbe kuwaita Israeli wote na Yuda, pia akaandika barua kwa Efraimu na Manase, kuwakaribisha ili waje hekaluni mwa Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu kuadhimisha Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda pia; akawaandikia nyaraka Efraimu na Manase, waje nyumbani kwa Bwana Yerusalemu, ili wamfanyie pasaka Bwana, Mungu wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Hezekia aliwatumia ujumbe watu wote wa Israeli na Yuda, na pia akawaandikia barua wenyeji wa Efraimu na Manase, akiwaalika wote waje katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu Yerusalemu, ili kuiadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa heshima yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akatuma ujumbe kuwaita Israeli wote na Yuda, pia akaandika barua kwa Efraimu na Manase, kuwakaribisha ili waje hekaluni mwa BWANA huko Yerusalemu kuadhimisha Pasaka kwa BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akatuma ujumbe kuwaita Israeli wote na Yuda, pia akaandika barua kwa Efraimu na Manase, kuwakaribisha ili waje hekaluni mwa bwana huko Yerusalemu kuadhimisha Pasaka kwa bwana, Mungu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda pia; akawaandikia nyaraka Efraimu na Manase, waje nyumbani kwa BWANA Yerusalemu, ili wamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Hezekia aliwatumia ujumbe watu wote wa Israeli na Yuda, na pia akawaandikia barua wenyeji wa Efraimu na Manase, akiwaalika wote waje katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu Yerusalemu, ili kuiadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa heshima yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia akatuma kwa Waisiraeli na kwa Wayuda wote, nao Waefuraimu na Wamanase akawaandikia barua, waje Yerusalemu Nyumbani mwa Bwana Mungu wa Isiraeli kula sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda pia; akawaandikia nyaraka Efraimu na Manase, waje nyumbani kwa BWANA Yerusalemu, ili wamfanyie pasaka BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Hezekia akawatumia ujumbe watu wote wa Israeli na Yuda, na vilevile akawaandikia barua watu wa kabila la Efuraimu na Manase, akiwaalika wote wakuje katika nyumba ya Yawe kule Yerusalema, kusudi wafanye sikukuu ya Pasaka kwa heshima ya Yawe, Mungu wa Israeli.